COUNCIL OF CONTRACTOR ASSOCIATIONS; TAARIFA KWA UMMA

  • Category: news
  • Published: Saturday, 16 November 2019 13:42
  • Written by Super User
  • Hits: 350

TAMKO LA BARAZA KUHUSU KUSIKITISHWA NA VITENDO VYA KUINGILIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMMA NA KUWAWEKA NDANI KIJINAI MAKANDARASI BILA KUZINGATIA MIKATABA.

Baraza la Vyama vya Makandarasi (The Council of Contractor Associations – CCA) linasikitishwa na ongezeko la matukio ya kuingilia utekelezaji wa miradi ya umma na kuwaweka ndani kijinai makandarasi bila kuzingatia mikataba ya miradi hiyo. Tumesikia katika vyombo vya habari juu ya:

1.Uamrishaji wa mabadiliko ya muda wa utekelezaji au mabaliko mengine bila kuzingatia mikataba iliyoko.

2.Utumiaji wa wa madaraka kutoa maagizo au kuwakamata wakandarasi na kuwaweka ndani kijinai, badala ya kutumia vifungu vya mikataba ya ukandarasi kutatua matatizo yanayo jitokeza.

3. Kutumia vitisho na kuwadhalilisha makandarasi.

Tunatambua shaukuya viongozi wa Umma kuona miradi inatekelezwa kwa ufanisi na kwa muda mfupi iwezekanavyo.

Hata hivyo tunatambua pia kwamba kazi za ujenzi haziendeshwi kijinai, bali kwa kuzingatia mikataba ya kisheria ambayo ikivurugwa, huharibu utekelezaji wa miradi hiyo na pia huharibu mazingira ya kufanya biashara ya ujenzi na sekta ya Umma kwa ujumla. Tunaiomba serikali na taasisi zake kuwasihi viongozi wa Umma kuwatumia wasimamizi wataalamu (Consultants) kutekeleza mambo yote yanayohusu miradi kwa kuzingatia mikataba husika.

Baraza la Wakandarasi wote kwa ujumla wataendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ufanisi na kwa muda muafaka na mara zote, kutumia vipengele vua mikataba ya miradi husika kushughulikia migogogro yake.

Imetolewa na;

  • Tanzania Civil Engineering Contractors Association
  • Association of Citizen Contractors
  • Contractors Association of Tanzania

About Company

The services embrace most aspects of environmental management, agricultural project, Eco-tourism, Engineering projects, Industries developments, petroleum projects, education and awareness.

Business Hours

Mon – Fri
09:00 am : 08:00 pm

Saturday ( 1st & 4th )
09:00 am : 08:00 pm

Subscribe Us & Receive Our Newslatter and Updates! Your Inbox Directly.

*We do not share your email id.